Kinyunga (Australia)

Kinyunga (au Kinoongar) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wanyunga katika jimbo la Australia Magharibi. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kinyunga 240. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kinyunga kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi. Wengine huangalia lugha zifuatazo kama lahaja za Kinyunga: Kibibbulman, Kigoreng, Kipinjarup, Kiwajuk na Kiwardandi.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search